Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MFUMO WA TAKWIMU HURIA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katik...

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katika Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ili aweze kuufungua mkutano huo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi umekuwa muhimu kwani unaleta uwazi pamoja na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wapili kulia meza kuu, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. Anayefuata ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue. 
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika.
 Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa makini wakati akitoa hotuba yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 barani Afrika unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani humo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika ndege ambayo inapaa bila rubani (Drone) na yenye uwezo wa kuchukua matukio mbalimbali ikiwa angani, wakati alipotembelea Banda la Buni Hub ambalo lipo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mtaalamu wa Benki ya Dunia, Frederick Mbuya akitoa elimu ya ndege hiyo kwa Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia kwa Rais Kikwete) pamoja na viongozi wengine walioambatana na Rais huyo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MFUMO WA TAKWIMU HURIA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MFUMO WA TAKWIMU HURIA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
http://1.bp.blogspot.com/-tGWO-vlTSLk/VemuIBawC5I/AAAAAAADX1w/L31M1b2nQVo/s640/PIX%2B2.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-tGWO-vlTSLk/VemuIBawC5I/AAAAAAADX1w/L31M1b2nQVo/s72-c/PIX%2B2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/rais-kikwete-afungua-mkutano-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/rais-kikwete-afungua-mkutano-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago