Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Mkutano wa Kampeni ya Mgombea CCM Urais wa Zanzibar Dk Ali Shein Viwanja vya Micheweni Pemba

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, akiwa na Mama Mwanamwema Shei...

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, akiwa na Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi wa CCM wakati wakiwasili katika viwanja vya mkutano wa Kampeni Micheweni Pemba kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni kugombea nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuomba ridhaa za Wananchi Pemba kumpigia kura za Ndio katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Sheinakisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano wa kampeni Wilaya ya Micheweni Pemba uikiwa ni mkutano wake wa Nne kisiwani Pemba katika kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kuomba kura. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Shein, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai wakiwa katika viwanja vya mkutano wa kampeni katika viwanja vya Jimbo la micheweni Pemba.
Mgombea Urais Zanzibar Dk Shein, akiwa na Viongozi wa CCM kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba wakifuatilia mkutano huo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Mohammed Aboud akihutubiwa katika mkutano huo wa kampeni viwanja vya micheweni Pemba.
Wananchi wa Wilaya ya Micheweni wakifuatilia mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja hivyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Mohammed Aboud akiwahutubia Wanachama wa CCM Jimbo la Micheweni wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na kuwataka Wananchi wa Micheweni kumpigia kura ya Ndio mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar katika viwanja vya Micheweni Kisiwani Pemba.
Mhe Zainab Omar akiwahutubia Wanachama wa CCM Wilaya ya Micheweni wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein uliofanyika viwanja vya Micheweni Pemba na kuwataka kutokupoteza nafasi hiyo ya kumchagua Dk Shein kwa maendelea ya Wananchi wa Zanzibar.
Mhe Ramadhani Abdalla Shabani akiwahutubia Wananchi wa Kisiwani Pemba wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar na kuwaambia msemaji wa uchimbaji wa mafuta Zanzibarb ni yeye hakuna mtu mwingine na suala hilo liko tayari kinachosubiriwa ni kupitisha sheria hiyo kuaza kazi ya uchimbaji wa mafuta Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai akiwahutubia Wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, na kusoma Ilani ya CCM jinsi inavyotekelewa katika miradi mbalimbali iliyoahidi wakati wa kipindi cha miaka mitano iliopita kwa kiasi kikubwa miradi hiyo imekamilika kwake na kulaani kitendo cha Wanachama wa CUF kuwashambulia Wanachama wa CCM wakirudi katika mkutano wa wa kampeni Chokocho na kusababisha kujeruhiwa kwa Mwanachama wa CCM na kuvunjwa kioo gari moja. 
Wanachama wa CCM Pemba wakishangilia Sera za CCM wakati wa Mkutano huo wa kampeni ya Urais wa Zanzibar katika viwanja vya Micheweni Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Micheweni Pemba akiwa katika mikutano yake ya Kampeni kisiwani humo mkutano huu ukiwa ni wa nne katika kuomba kura kuiongoza Zanzibar, Akisoma Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 jinsi ya kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar katika Sekta mbali mbali za Kijamii.   

Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar wakati wa mkutano wake wa Kampeni kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya Micheweni Pemba.

Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Pemba wakifuatilia hutuba ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya micheweni Pemba akiwa katika mkutano wake wa kampeni kisiwani humo kuomba kura kwa mara ya pili kuongoza Zanzibar kwa Maendeleo ya Wananchi wake kuwapatia maendeleo katika Sekta mbalimbali za Jamii.
Mwanachama wa CCM akishangilia wakati wa mkutano huo wa kampeni ya Urais katika viwanja vya micheweni Pemba.
Taswira wa Uwanja wa mkutano micheweni Pemba ilivyokuwa kwa Wanachama wa CCM wakimsikiliza Mgombea wa Urais 
Dk Shein.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Micheweni Pemba Ndg Shamata Khamis.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Wingwi Pemba Ndg Said Omar Said,. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Konde Pemba Ndg Omar Seif Abeid. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Tumbe Pemba Ndg. Ali Khamis. Bakar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Micheweni Pemba Ndg Khamis. Juma Bakar. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Wingwi Pemba Ndg Khamis. Shaame
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Konde Pemba Ndg Ramadhani Omar. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM katika Jimbo la Tumbe Pemba Ndg Rashid Kassim Abdalla. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwanbi katika Wilaya ya Micheweni Pemba kupitia Chama cha Mapinduzi, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya micheweni Pemba. 
Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba Wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Micheweni na kuwatambulisha Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kwa Wananchi.Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. Zanzinews,com

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Mkutano wa Kampeni ya Mgombea CCM Urais wa Zanzibar Dk Ali Shein Viwanja vya Micheweni Pemba
Mkutano wa Kampeni ya Mgombea CCM Urais wa Zanzibar Dk Ali Shein Viwanja vya Micheweni Pemba
http://2.bp.blogspot.com/-DEtJ0mBsk2o/Vf-RpOjv61I/AAAAAAAB-KI/MTtRgV8QFqI/s640/IMG_0322.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-DEtJ0mBsk2o/Vf-RpOjv61I/AAAAAAAB-KI/MTtRgV8QFqI/s72-c/IMG_0322.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/mkutano-wa-kampeni-ya-mgombea-ccm-urais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/mkutano-wa-kampeni-ya-mgombea-ccm-urais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago