Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MGOMBEA URAIS-CCM DR JOHN MAGUFULI:NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.

Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni,Korogwe vijijini. MGOMBEA ura...

Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni,Korogwe vijijini.
MGOMBEA urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.

Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.

Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo leo  katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe, Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini . PICHA NA MICHUZI JR-LUSHOTO,TANGA
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegeme.
  Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa hadhara  katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani Bumbuli kuwahutubia wananchi na kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
 Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kata ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.
Bangozzzz
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe mjini  Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa,Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani humo.
Wakazi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jioni ya leo,
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
Wananchi wakifuatilia mkutano.
  Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya umati wa wananchi  wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Togotwe.
Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia .

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MGOMBEA URAIS-CCM DR JOHN MAGUFULI:NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.
MGOMBEA URAIS-CCM DR JOHN MAGUFULI:NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.
http://3.bp.blogspot.com/-y9cijudAA1Y/VfCL2rwb4zI/AAAAAAAC-zg/j3rkdeDdE-c/s640/_MG_3872.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-y9cijudAA1Y/VfCL2rwb4zI/AAAAAAAC-zg/j3rkdeDdE-c/s72-c/_MG_3872.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/mgombea-urais-ccm-dr-john.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/mgombea-urais-ccm-dr-john.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago