Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JESHI LA MAGEREZA NCHINI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KATIKA KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI

  Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kutoka Magereza Mkoani tanga wakiendelea na majadiliano katika Kongamano h...

  Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kutoka Magereza Mkoani tanga wakiendelea na majadiliano katika Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku tatu.
-----
Na, Lucas Mboje, Morogoro 

Jeshi la Magereza nchini limeahidi kuendelea kushirikiana na Asasi ya Envirocare katika kuimarisha Madawati ya Msaada wa Kisheria Magerezani ili kuleta tija katika utatuzi wa changamoto ya Msongamano wa Mahabusu inayolikabili Jeshi hilo. Kauli hiyo imetolewa jana Mkoani Morogoro na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja alipokuwa Mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani na Mahabusi za Watoto. 

Jenerali Minja amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukulia kwa uzito stahiki suala la Msongamano wa Mahabusu Magerezani ikiwemo kushirikiana na Wadau wa Haki Jinai katika kupunguza changamoto ya Msongamano wa Mahabusu Magerezani. "Napenda kutoa rai kwa Asasi zingine zenye malengo yanayofanana na Asasi hii nazikaribisha kuja kufanya kazi na Jeshi la Magereza kwani mwelekeo wa Jeshi kwa sasa ni Urekebishaji wa Wafungwa(From Prisons to Corrections) ambapo Jeshi la Magereza watafanya kazi kwa karibu na Asasi za Kiraia na Jamii kwa ujumla". 

Alisema Jenerali Minja. Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Envirocare, Bi. Loyce Lema amesema kuwa imekuwa ni faraja kwao kupata ushirikiano kama huo kutoka Jeshi la Magereza kwani umewezesha kutekelezwa kwa mradi huo wa kutoa Msaada wa Kisheria kwa Mahabusu waliopo Magerezani kwa matokeo chanya kwa muda mufupi. Bi. Lema alisema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa miaka mitatu(2012 - 2015) na umetekelezwa kwenye Magereza 20 na Mahabusu 04 za Watoto katika Mikoa 05 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam. 

 Asasi ya Envirocare kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza ilifanya utafiti wa awali wa kuangalia hali halisi ya Msongamano katika Magereza yaliyopo katika Mikoa mitano ya mradi. Matokeo ya jumla ya utafiti huo yalionesha kuwa kuna tatizo kubwa la Msongamano ambao unasababishwa na idadi kubwa ya Mahabusu katika Magereza ya Mikoa hiyo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JESHI LA MAGEREZA NCHINI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KATIKA KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI
JESHI LA MAGEREZA NCHINI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KATIKA KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI
http://1.bp.blogspot.com/-3axyt6yrKFE/VehdYXnESmI/AAAAAAADXv0/OaGnuLj0JYY/s640/photo%2B2.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-3axyt6yrKFE/VehdYXnESmI/AAAAAAADXv0/OaGnuLj0JYY/s72-c/photo%2B2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/jeshi-la-magereza-nchini-kushirikiana.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/jeshi-la-magereza-nchini-kushirikiana.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago