Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

BENKI YA DUNIA YAIDHINISHA DOLA ZA MAREKANI MILLIONI 80 KUJENGA AJIRA TANZANIA

  Bodi ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia leo wameidhinisha  mkopo wa   maendeleo wa Dola za Marekani milioni 80 zinazolenga...

  Bodi ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia leo wameidhinisha  mkopo wa 
 maendeleo wa Dola za Marekani milioni 80 zinazolenga kuboresha utendaji katika sekta binafsi ya Tanzania, ili kukuza wajibu wake katika kujenga ajira nchini.
 
Kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, uwekezaji wa sekta binafsi ulikuwa umejikita  zaidi katika sekta chache zinazokua kwa kasi, kama vile sekta za madini, fedha, mawasiliano na uchukuzi, wakati sekta zinazohitaji nguvu kazi nyingi kama vile kilimo na uzalishaji viwandani zilikua kwa kiwango chini ya wastani wa uchumi  (takribani asilimia 7 mwaka 2014/15). Matokeo yake ni kwamba ajira hazikuongezeka kwa kasi inayolingana na kukua kwa idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi.

“Maelfu ya vijana wanaingia katika soko la ajira kila mwaka na wanakuwa na ari na matumaini makubwa,” anasema Bi. Bella Bird, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini. “Kujenga ajira zenye tija ni kipaumbele kwa Tanzania, na ni sekta binafsi pekee ndiyo inayoweza kuzalisha idadi ya ajira zinazotakiwa. Mageuzi ya sera yanayofadhiliwa na mradi huu yatasaidia kupunguza vikwazo vya kufanya biashara nchini, kuruhusu sekta binafsi na ukuaji wa ajira.”

Kila mwaka, takribani vijana 800,000 wanaingia katika soko la ajira, ambalo linatarajiwa kukua kutoka watu milioni 20 leo hadi watu milioni 40 ifikapo mwaka 2030. Fursa za kazi zenye tija kwa vijana hawa bado ni finyu, nyingi zikiwa katika sekta isiyo rasmi.

Mazingira ya Kazi kwa ajili ya Shughuli za Sera ya Kuendeleza Ajira ni programu ya kwanza katika mfulululizo wa programu tatu za shughuli za msaada wa bajeti kwa Tanzania. Shughuli hii inajenga juu ya programu inayoongozwa na serikali ya ‘Matokeo Makubwa Sasa’ (BRN), na inasaidia programu kadhaa za sera zinazolenga katika kuboresha kwa ujumla ‘urahisi wa kufanya biashara’ na kuimarisha masoko ya vipengele vikuu (nguvu kazi, ardhi na mtaji). Aidha, shughuli hii inasaidia maboresho yanayolenga kuinua mazingira ya biashara katika biashara ya kilimo na utalii, sekta mbili zinazotoa ajira nyingi ambazo ni muhimu kwa Tanzania.

Tunaunga mkono hatua madhubuti za kurahisisha maisha ya biashara,” anasema Andrea Dall’Olio, Kiongozi wa Kikosi Kazi cha Benki ya Dunia. “Kwa mfano, tuliainisha ada, ushuru na kodi zaidi ya 59 zinazotozwa kwenye sekta ya utalii na wakala mbalimbali wa serikali. Orodha kamili inaweza kupatikana katika tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, na tunaendelea kufanya kazi na serikali kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi yao na athari zake kwenye biashara.”

Shughuli hii ya Kuendeleza Sera ya Ajira imetayarishwa kwa pamoja na Shirika la JICA (Japan International Cooperation Agency), ambalo limepanga kutoa fedha sambamba na Benki ya Dunia.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: BENKI YA DUNIA YAIDHINISHA DOLA ZA MAREKANI MILLIONI 80 KUJENGA AJIRA TANZANIA
BENKI YA DUNIA YAIDHINISHA DOLA ZA MAREKANI MILLIONI 80 KUJENGA AJIRA TANZANIA
http://3.bp.blogspot.com/-mWxFtseUnCI/VemmwFkO3BI/AAAAAAADX0k/XgMi7k2wO4c/s1600/logo_worldbank_baru.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-mWxFtseUnCI/VemmwFkO3BI/AAAAAAADX0k/XgMi7k2wO4c/s72-c/logo_worldbank_baru.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/benki-ya-dunia-yaidhinisha-dola-za.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/benki-ya-dunia-yaidhinisha-dola-za.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago