Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa wakati watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliposimamisha daladala eneo la Jangwani na kuingia ndani kupora mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha.

Askari na wasamaria wema wakiwa wamebeba mwili wa abiria aliyepigwa risasi na majambazi akiwa ndani ya daladala eneo la Jangwani, Dar...


Askari na wasamaria wema wakiwa wamebeba mwili wa abiria aliyepigwa risasi na majambazi akiwa ndani ya daladala eneo la Jangwani, Dar es Salaam jana. Daladala hilo lilikuwa likitoka Kariakoo likielekea Ubungo Mawasiliano. Picha na Edwin Mjwahuzi 
----
By Hadija Jumanne na Pamela Chilongola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa wakati watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliposimamisha daladala eneo la Jangwani na kuingia ndani kupora mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha.

Watu hao, waliokuwa na pikipiki aina ya boxer, walikuwa wakifuatilia basi hilo linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mwenge na kulisimamisha eneo la Jangwani saa 7.30 mchana na baadaye kuwaamuru abiria wote wainame kabla ya kuelekea kiti cha nyuma alikokuwa amekaa mtu huyo aliyekuwa amebeba mkoba.

Mmoja wa abiria wa daladala hilo, Rehema Michael alisema wakati basi lao likiwa linaenda taratibu, alimuona mtu aliyekuwa amepakizwa kwenye pikipiki akishuka na kumfuata dereva na kisha kumuelekezea bastola usoni, akimtaka asimamishe gari.
Alisema dereva wao alitaka kukunja kona kuelekea Jangwani, lakini akatii amri na ndipo dereva wa bodaboda alipokwenda nyuma ya daladala na kumtaka mmoja wa abiria aliyekuwa amekaa nyuma ya daladala kutoa begi, huku mwingine akipiga risasi hewani, lakini hakupewa mkoba huo.

“Baada ya kuona yule abiria anakaidi  agizo lao, mmoja wa majambazi hao alimpiga risasi ya kichwani na kifuani na kuanguka chini huku yule abiria mwenzake ambaye alipewa begi hilo alishike alilitupa chini na mmoja wa majambazi aliingia ndani ya daladala na kulichukua,” alisema Hashim Ally mkazi wa Manzese.

Shuhuda mwingine, Richard Urio alisema wakati uvamizi huo ukitokea abiria walikuwepo ndani ya daladala hiyo akiwemo konda walilazimika kulala chini baada ya kusikia milio ya risasi zilizokuwa zikipigwa hewani, na kwamba baada ya kuchukua lile begi walimpiga risasi abiria mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu baada kuhisi alikuwa akizuia begi lisitolewe.

“Siti ya nyuma walikuwa wamekaa abiria wanne, na wawili kati yao walikuwa wamasai ambao mmoja wapo alikuwa amevaa begi mgongoni ambalo lilichukuliwa na majambazi baada ya kumuua mmoja wa wamasai huku mwingine akijeruhiwa na bastola shavuni,” alisema Urio.

Shuhuda mwingine, Regina Mateso alisema yeye alipanda daladala hiyo eneo la Shakilango  na kuwakuta wamasai hao ambao inasemakana walikuwa na fedha nyingi kutokana na maongezi yao.

“Wale wamasai walikuwa wanapigiana mahesabu na wapi kwa kwenda kubadilisha fedha. Yule aliyefariki alikuwa anamwambia mwenzake ukibadilisha hizi dola unapata Sh16 milioni, hivyo inawezekana wale abiria walikuwa na kiasi hicho cha fedha ambacho walikuwa wameweka katika begi la mgongoni,” alisema Mateso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala, Lucas Mkondya alisema tukio hilo limetokea na wanalifanyia  kazi .

“Na sisi polisi tumelipata sasa hivi ndio kwanza tunalifanyia kazi likikamilika tutatia taarifa,”alisema MkonyaHata hivyo, alipopigiwa simu baadaye kupata taarifa kamili alisema yuko kwenye mkutano.Mwili wa abiria huyo ulipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na abiria aliyejeruhiwa.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa wakati watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliposimamisha daladala eneo la Jangwani na kuingia ndani kupora mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha.
Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa wakati watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliposimamisha daladala eneo la Jangwani na kuingia ndani kupora mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha.
http://2.bp.blogspot.com/-q67fwWsFMn8/VeLfY_aRcwI/AAAAAAADXVQ/LQUhosJhNgg/s640/majambazi.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-q67fwWsFMn8/VeLfY_aRcwI/AAAAAAADXVQ/LQUhosJhNgg/s72-c/majambazi.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/08/mtu-mmoja-amefariki-dunia-na-mwingine.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/08/mtu-mmoja-amefariki-dunia-na-mwingine.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago