
Wakaanga samaki katika Soko la Feri Magogoni, Dar es Salaam wakiendelea na shughuli hizo kwenye moshi unaotokana na kuharibika kwa vitolea moshi na kusababisha moshi huo kutanda hivyo inayowalazimisha kila wakati kutoka nje ili kupata hewa safi. Baadhi ya majiko yaliteketea kwa moto mwezi kama huu mwaka jana katika soko hilo na kwa mujibu wa mmoja wa wakaanga samaki hao, Mfaume Namkopa, kuna jumla ya wakaanga samaki 143 wanaotumia kwa zamu majiko yaliyobakia na kusababisha usumbufu mkubwa.Picha na Mohamed Mambo

