H@ki Ngowi: Wahitimu Shahada Ya Uzamili Ya Usimamizi Wa Biashara Za Kimataifa H@ki Ngowi: Wahitimu Shahada Ya Uzamili Ya Usimamizi Wa Biashara Za Kimataifa
Mkurugenzi wa Chuo Cha Biashara za Nje cha Nchini India (IIFT) Thomas Chako akiongea katika mahafali ya 12 ya Shahada ya Uzamili inayotolewa na chuo hicho kwa ushirikiano na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM ) cha Dar es salaam. Chako alikabidhi veti kwa wahitimu takribani 31. Wengine pichani kutoka kulia ni Makamu wakuu wa Chuo cha IFM Prof. Jairo na Prof. Tadeo Satta na Mkuu wa Chuo hicho Prof Godwin Mjema. Chako alihimiza umuhimu wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa kutosha wa biashara za kimataifa ili kunufaika na fursa za biashara za ulimwengu.
Mathew Shayo(Kulia)akipokea cheti chake cha kuhitimu shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara za kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Biashara za Kimataifa cha India (IIFT) kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho. Thomas Chako katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. IIFT huendesha kozi hiyo ya MBA-IB kwa ushirikiano na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Makamu wakuu wa Chuo cha IFM, Profesa Isaya Jairo (wa pili kulia) na Profesa Tadeo Satta. Chako alihimiza umuhimu wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa kutosha wa biashara za kimataifa ili kunufaika na fursa za biashara za ulimwengu.

0 comments:

Clouds FM Live

Follow by Email

Blog Archive

Popular Posts

MATANGAZO

Followers

How to make a Website