Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza wakati akizinduzia Tume ya Utumishi wa Bunge jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mhe. Mizengo Pinda
 Waziri Mkuu akimkabidhi Spika wa Bunge cheti cha Utumishi bora.
 Waziri Mkuu akimkabidhi cheti cha Utumishi bora kwa Bunge la tisa Mbunge Viti  Maalum Mhe. Kidawa Saleh.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi cheti cha Utumishi bora Kamishna Mstaafu na Mpya Mhe. Abdulkarim Shah.
 Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliohudhuria Uzinduzi huo.
 Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Wajumbe wa Tume iliyomaliza muda wake, Tume Mpya, Menejimenti na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
--
WAZIRI  Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda ameitaka Tume ya  Utumishi Bungeni  kujumuisha wajumbe wengine ambao siyo wabunge wenye ujuzi na uzoefu wa maeneo kama sheria,utumishi na utawala  ili kuleta ufanisi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Tume ya Utumishi Bungeni.  

Amefafanua kuwa muundo wa Tume ulioainishwa kwenye Kifungu cha 12 cha Sheria ya Utumishi wa Bunge ya mwaka 2008 umejumuisha  wajumbe 11 wote wakiwa ni wabunge.

Aidha amesema pamoja na wabunge kuwa wajumbe wa Tume hiyo bado yapo maeneo yenye mgongano wa kisheria  na katiba ambayo  yanaweza kusaidiwa na wataalam katika kutekeleza majukumu ya tume hiyo.

“Yapo maeneo yana mgongano wa kisheria wa Katiba na Sheria ya Utumishi wa Bunge,Kwa Mfano kifungu cha sheria ya utumishi wa Bunge kinaainisha kuwa Tume itapendekeza majina matatu ya watu ambayo inaona wanafaa kuteuliwa kuwa katibu wa Bunge kinyume na Masharti ya Ibara ya 87 ya katiba ambayo inasema kuwa katibu wa Bunge atateuliwa na Rais kutoka miongoni  mwa watumishi waandamizi.”Alisema Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa maeneo kama haya na mengineyo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuepuka migongano kiutendaji na hivyo kuzuia dalili zozote za ukiukwaji wa katiba.

Amesema kuwa Tume hiyo inapaswa siyo tu kuyaendeleza na kuyakamilisha majukumu ya Tume iliyomaliza muda wake bali pia kubuni maeneo mengine mapya yatakayolinufaisha bunge la kumi kwa kuzingatia kanuni zilizopo.  


Imeandikwa na Beatrice Mlyansi-MAELEZO            

0 comments:

Sikiliza Clouds FM LIVE

Nifwate Kwenye Twitter

Sheria Ngowi Designs Online Bookings

Google+ Badge

Google+ Followers

Followers

Translate

Blackberry Application


A.V.I.D


Follow by Email

Blog Archive

Mimi na Tanzania

Skylight Band

Grooveback


How to make a Website