Mhariri Kubenea
Mgonjwa...

MHARIRI Mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea Pichani aliyemwagiwa kumwagiwa tindikali ofisini kwake akiwa na Mhariri Mshauri Ndimara Tegambwage,Hivi karibuni ameshindwa kutoa ushahidi wake katika kesi iliyoko mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam Leo,kutokana na kuwa mgonjwa.Mwendesha Mashitaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Kenyela aliieleza mahakama hiyo kuwa Kubenea aliyekuwa atoe ushahidi wake jana dhidi ya watuhumiwa sita waliovamia ofisi yake iliyopo Kinondoni, alishindwa kutoa ushahidi wake kutokana na kutojisikia vizuri na kesho anatarajiwa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.Habari hii na Maulid Ahmed.
Toleo La Raia Mwema Wiki Hii..
**Mawaziri wengine kwenda na maji.

ILI kukwepa makosa ya kiuteuzi, Rais Jakaya Kikwete sasa ameamua kuwachunguza mawaziri wake wote na wanasiasa ambao wanatarajiwa kuwamo katika timu yake ijayo, Raia Mwema imeambiwa.
Habari za wiki hii zinasema hatua hiyo ya Rais Kikwete inalenga kukwepa makosa kama yaliyofanyika katika uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge,ambaye tangu mwanzo uteuzi wake ulikuwa ukitiliwa shaka na umma.Mjengwa,Ayub Rioba na Padri Privatus Karugendo na nyingine nyingi liperuzi gazeti hili matata kabisa kwa kubofya Hapa
Vibwanga Vya Tabata
Leo..
Wakazi wa maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam,wakichungulia ndani ya gari kumuangalia msichana Rehema Kefa (18) anayedaiwa kuwa ni mchawi baada ya kukamatwa akiwa katika Zahanati akidai kutafuta mtoto na damu ya kunywa.
Ofisa wa ngazi ya juu kutoka jeshi la Polisi akimhoji Msichana Rehema Kefa (18)kwenye kituo cha Polisi cha Buguruni jijini Dar es Salaam baada ya Msichana huyo kukamatwa akiwa katika Zahanati moja iliyoko Tabata akiwa katika harakati za kutafuta mtoto kwa nia ya kunywa damu yake.Lakini Msichana Rehema alipokuwa anajieleza baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha Polisi Buguruni,jijini Dar es Salaam leo alidai yeye ni mkazi wa Tabata Msimbazi na kukiri kuwa alifika katika Kituo cha Afya Tabata kwa agizo la bibi yake.Picha zote kwa Msaada wa Mpiga Picha Maalum wa TSN na Mdau Mpoki Bukuku.
Breaking News..
Matokeo ya Urais Zimbabwe
Tsvangirai 47%,
Mugabe 43%
Pichani ni Kiongozi Mkuu wa chama cha Upinzani nchini Zimbabwe(MDC) Morgan Tsvangirai akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Matokeo Ya uchaguzi yaliyorudiwa
kuhesabiwa kwa mara ya pili kumpa ushindi wa 47% na kumpita Mpinzani wake Mkuu Rais Wa sasa Robert Mugabe Kutoka chama cha ZANU-PF aliyeambulia 43%,kwa Habari zaidi Bofya Hapa na Hapa
Mchawi Mwingine abambwa
Tabata..

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Rehema Kefa (18) akiwasilisi katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam,baada ya kukamatwa akiwa katika Zahanati moja iliyoko Tabata akiwa katika harakati za kutafuta mtoto na kunywa damu yake.Msichana huyo,alikamatwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kukiri kuwa ameanza kufanya kazi zinazodaiwa kuwa ni za kichawi akiwa na miaka mitano.
---------
Siku tatu tu baada ya kijana kukamatwa na kichwa cha mtoto, kijana mwingine, safari hii msichana, amekamatwa katika hospitali ya Tabata iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kwa tuhuma za kutaka kuiba mtoto wodini.
Rehema Kefa(18) Mkazi wa Mkuranga alikutwa akitaka kumtorosha mtoto huyo leo aliyekuwa katika wodi ya mateniti hospitalini hapo leo.
Inasemekana Rehema alibambwa na nesi wa zamu katika wodi hiyo ambaye ni mlokole, ambaye baada ya kuona mauzauza ya huyo msichana inasemekana alifanya maombi, na mtuhumiwa huyo akaanza kutambaa kama nyoka wodini hapo.
Polisi waliitwa na kumpeleka Rehema kituo kidogo kilichopo karibu na hospitali hiyo ambako alikiri kwamba yeye ni mtu wa juju, na kudai kwamba shughuli hiyo kafundishwa na bibi yake kwa jina la Salome Nganame.
Aliwaambia askari kwamba hakuwa peke yake katika skuli hiyo, kwani mafunzo hayo ya undondocha kafunzwa yeye na kinadada wengine aliowataja kama Asha Said(29), Fatuma Saleh(23) na Khadija Mpogolo.
Alisema yeye na hao aliowataja ilikuwa waibe pamoja mtoto pele hospitali na kwenda kumnyonya damu.
aliwaambia askari kwamba walipomkamata bibi huyo na wenzie walikuwa wanaw
acheki tu kwenye 'TV' yao huko waliko.Picha na Mpiga Picha Maalum wa TSN.
Waziri Mkuu Pinda awasili
Iringa ...

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (nyuma yake) wakisalimiana na wenyeji wao walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa kwa ajili ya sherehe za Mei-Mosi kitaifa zinazofanyika mkoani Iringa Kesho..
CCM ndio Waasisi-
Adam Mzee
Mjumbe wa CCM Taifa ndg. Nape M. Nauye(kushoto)Adam Mzee(Mwenyekiti CCM Mysore)na EdwardNyange(Katibu Mwenezi CCM Mysore)
Vijana wa CCM Mysore walisheherekea siku ya muungano kwa hari kubwa ya kutaka kuleta mabadiliko ya kweli nchini kwao, akihutubia Vijana hao Ndg.Nape Nauye,mjumbe wa CCM taifa alisema...'VIJANA TUAMKE NA KUJADILI JUU YA TANZANIA TUNAYOITAKA.CCM BADO NI CHAMA IMARA LICHA YA MISUKOSUKO INAYOKIKUMBA SASA KUTOKANA NA BAADHI YA MAKADA KUKUMBWA NA KASHFA MBALIMBALI KAMA ZA UFISADI..MUUNGANO NI MOJA YA MATUNDA AMBAYO CCM INAJIVUNIA SANA LEO KWANI NI SERA YAKE NA NDIO WAASISI.'
''KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI''
By
Adam Mzee
Mwenyekiti wa CCM
Mysore.
Da' Chemi..
Da Chemi (kushoto)akiwa na Mcheza sinema,Jamal Mixon kwenye set ya Mall Cop ndani ya Burlington Mall,Paul Blart:Mall Cop ambayo itakuwa sinema ya vichekesho (Comedy).
Kipanyaa..

Ronaldo Azua Balaa..
Pichani ni Carla mmoja wa walimfanyia varangati Ronaldo akitoa maelezo Polisi huku mwenzie Andrea akiwa Ndani ya gari.
-----------
Mchezaji mahiri wa kimataifa wa Brasil Ronaldo amepatikana na janga jingine kuhusiana na ukware, Ronaldo amepigana na "malaya" watatu alioingia nao kwenye chumba cha Motel yake baada ya kugundua kuwa hawakuwa wanawake bali ni wanaume waliojibadilisha kuwa wanawake (pichani juu)kwa mengi zaidi juu ya Habari hii bofya Hapa
Rais Kikwete akutana
na Tsvangirai..
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto)akisalimiana na Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini Zimbabwe,The Movement for Democratic Change(MDC)Bw Morgan Tsvangirai jana jijini Addis Ababa wakati viongozi hao walipokutana kwa mazungumzo ya faragha katika hoteli ya Sheraton.
Banjuka Night ndani ya
Reading
Tigo Lotto..
Meneja Masoko wa Tigo Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto)akikabidhi fedha taslimu shilingi Milioni moja kwa mkazi wa Dar es Salaam Bw Salum Said aliyekuwa miongoni mwa washindi wa kila wiki wa promosheni ya Tigo Lotto Zawadi kwa washindi, zilikabidhiwa jijini Dar es Salaam Jana.
Makala Ya Leo..
*Serikali isikumbatie Wawekezaji Wababaishaji..

SERIKALI imeamua kuikopesha kampuni ya (TRL) Sh.bilioni 3.6 kwa miezi mitano sawa na Sh milioni 700 kila mwezi ili iweze kuwalipa wafanyakazi wake., baada ya kudai kuwa haina uwezo wa kuwalipa kima cha chini Sh.160,000 hali iliyosababisha wafanyakazi kugoma.
Imefikia hatua hiyo ,baada ya kampuni hiyo kudai kuwa haina uwezo kuwalipa wafanyakazi wake kima chini sh 160,000.Hali iliyosababisha wagome kufanya kazi.
Aliyetangaza kuikopesha TRL ni Waziri MKuu, Mizengo Pinda ,wakati akijaribu kumaliza mgogoro wa mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.Hapa nadhani Pinda alilazimika kukubali serikali kubeba mzigo huo ili kuwalainisha wafanyakazi warejee kazini.Pinda alilazimika kuingilia mgogoro wa wafanyakazi na menejimenti ya TRL baada ya wafanyakazi hao kugoma mwanzoni mwa mwezi huu wakidai makato ya mshahara wao.kwa mengi zaidi juu ya makala hii ya leo,mtembelee happiness Katabazi kwa kubofya Hapa
Kombe la Muungano...
Waziri wa Michezo na Utamadanu Bw. George Mkuchika akikagua timu ya soka ya Unilever katika mashindano ya Kombe la Muungano yanayofanyika Mufindi, Iringa.
Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,George Mkuchika akipiga penelti ikiwa ni ishara ya ufunguzi Rasmi wa mashindano ya Kombe la Muungano kwenye Uwanja waIgowole, Mufindi, mkoani Iringa
Rais Kikwete ateta na
Wafanyakazi,
AU..
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa Pili kulia,akiongea wafanyakazi katika Makao Makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa Ehiopia leo.Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja huo,Jean Ping na kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania Bernard Membe.Rais Kikwete,anatarajiwa kukutana na Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika.
Baadhi ya watumishi wanaofanya kazi katika Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) iliyopo jijini Addis Ababa Ethiopia wakimsikiliza kwa Makini Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anaongea nao leo katika Makao makuu ya umoja huo Addis Abba Ethiopia.
Mazishi Ya Mtoto
Salome...
Upendo Danstan,Mama mzazi wa,Salome Yohana,aliyechinjwa na mtuhumiwa Ramadhani Mussa wiki iliyopita,akisaidiwa baada ya kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mwanawe, aliyezikwa katika makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.
Upendo Danstan, mama mzazi wa, Salome Yohana,aliyechinjwa na mtuhumiwa Ramadhani Mussa wiki iliyopita,akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mwanawe, aliyezikwa katika makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.
Wazazi wa Salome Yohana aliyekutwa amekufa siku ya Jumamosi na baadae kichwa chake kukutwa kikinyonywa damu juzi na Ramadhani Mussa,wakizika mwili wa mtoto wao leo jioni kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Umati wa waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni kabla ya kuelekea kwenye Mazishi ya Mtoto Salome (3) aliyezikwa leo kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam,Mwenyezi mungu ailaze roho ya Marehemu Salome mahala pema peponi Ameni.Picha Zote kwa Msaada Mkubwa wa Mpoki Bukuku The Citizen na Bernard Rwebangira kutoka TSN.
Ayoub Mzee..

Mr Ayoub Mzee (Right) with the UK Home office minister for Immigration
Hon Meg Hillier MP.
Undani zaidi Juu ya Kifo Cha
Mtoto Salome..
Pichani juu ni kijana Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo kwenye hospital ya taifa ya muhimbili Hivi karibuni.
Picha juu kulia aliposimama Mdau,ni sehemu inayoaminika kuwa mtoto
Salome alichinjwa..
---------
Mauaji ya kikatili ya kuchinjwa kama kuku mtoto pekee kwa wazazi wake, Salome Yohana (3) yameumiza wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na hata nje ya jiji na vitongoji vyake na wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kitendo hicho.
Akimsimulia mwandishi wetu jinsi Salome alivyotoweka nyumbani na kukutwa amechinjwa, mama mzazi wa mtoto huyo, Upendo Dustan (27) alisema kuwa siku hiyo ya Ijumaa wiki iliyopita majira ya saa 2.00 usiku aliandaa chakula wakala na mwanaye ambaye baadaye alikwenda kucheza nje na mtoto wa jirani yao.Kwa habari hii zaidi juu ya tukio hili la kusikitisha bofya Hapa
Uchaguzi Chuo Kikuu
Wadororaa..
KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong’ Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.
Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.
Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura.Habarii hii na Jackson Odoyo na Christopher Maregesi.
Mambo ya Precision
Air..
Abiria wakipanda ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Precision katika hafla ya uzinduzi wa ndege hiyo iliyoanza safari zake zanzibar,Mwanza Dar es Salaam jana jijini Dar es Salaam.Picha na Bernard Rwebangira.
Filamu zinazowania tuzo za
Vinara 2007/08..
-----------
Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.

Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.
Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.

Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.

Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.

Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.

Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.
Mtoto aliyekatwa kichwa
Kuzikwa Leo..
Pichani Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo
kwenye hospital ya tIafa ya muhimbili Hivi karibuni.Kwa sasa bado anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi..
----------
MTOTO Solome Majana (3) aliyefariki wiki iliyopita katika mazingira ya kutatanisha baada ya kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili chake anazikwa leo makaburi ya Tabata. Akizungumza na majira jana baba wa mtoto huyo, Bw. Yohana Majana (26),alisema wamekamilisha taratibu zote za kipolisi na waliruhusiwa kuchukua mwili huo wakati wowote kuanzia jana asubuhi.
"Tumemaliza taratibu zote za polisi na leo (jana asubuhi) tulikubaliana kuwa muda wowote tukiwa tayari tuuchukue mwili wa marehemu kwa maziko, tumeruhusiwa kufanya hivyo."alisema Akizungumzia mkasa huo alisema serikali inatakiwa kuamini kuwa uchawi upo na watu wanaobainika kuhusika katika matukio ya kichawi kama lililomtokea kwa mwanae Salome, wawajibishwe.
Bw. Majana, alisema yapo matukio mengi ambayo yanatokea ambayo yanahusika na masuala ya uchawi lakini kutokana na Serikali kutotilia mambo yamekuwa yakienda hivi hivi na watu wengi kuathirika. Alisema mtoto wao Salome alitoweka nyumbani Aprili 25 mwaka huu jioni na kesho yake walikuta mwili wake ukiwa umekatwa kichwa.Habari hii na Eben-Ezery Mende
Mkutano wa Shina la CCM -Reading
Uingereza
May 4th..
------
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wanachama Wote - C C M - Reading
Wakereketwa Wote - C C M - Reading
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote wa Reading
Tarehe: 04/05/2008 Saa: 08:00 Mchana - Saa 12:00 Jioni
WAPI:
UKUMBI WA: 79 (Kijiweni)
79 LONDON ROAD
READING
RG1 5BY
Watanzania ambao wangependa kujiandikisha,mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).
Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:
MAIRA MIGIRE – 07799212095
Katibu wa CCM Shina la Reading
Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Nyama choma na Muziki Baada ya Shughuli Zote.
Kiingilio – BURE!!!
Kipanya..

LONDON SCHOOL OF
COMMERCE ..

Ndugu wananchi (wadau), Chuo cha LONDON SCHOOL OF COMMERCE (associate college of university of wales) kinatangaza usajili maalumu wa wanafunzi wapya wa mwaka huu wa masomo 2008/9 unaoanza mwezi wa sita (June) 2008.
Kwa taarifa zaidi na kozi mbalimbali wanazotoa tembelea tovuti yake www.lsclondon.co.uk .Kuna punguzo maalumu la Ada kutoka £6450 mpaka £3950 kwa mwaka wa masomo huu kwa wanafunzi wa kitanzania watakaopitia kwangu kuomba na kukubaliwa masomo yao hapa chuoni, punguzo hili maalumu utalipata kwa kuwasiliana nami ili nikuwakilishe hapo chuoni.
Naomba wanafunzi wenye interest na kusoma chuoni hapa kwa kozi zilizotangazwa kwenye tovuti ya chuo tuwasiliane kwa namba yangu hii hapa +447506458289.... au email hii (ally.abdallah@lsclondon.co.uk).... Natoa tahadhari kwamba Mimi ni wakala wa wanafunzi wa kitanzania ninayehusika na punguzo la bei tu.
Sihusiki kabisa na upatikanaji wa kibali cha kuingilia Nchini (visa), kwahiyo naomba nisiulizwe maswali kuhusu swala hilo,chuo kitakamilisha kila taratibu za mwanafunzi aliyekubaliwa masomo na kupata nafasi chuoni ili eweze kupata visa..
kwa maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa visa za uingereza bofya hapa http://www.ukvisas.gov.uk/en/Ni matarajio yangu, kila mwenye kutaka kupata habari zaidi za kusoma chuoni hapa na punguzo hili la bei atapitia tovuti ya chuo kwanza ili kumaliza mushkeli aliokuwa nao, kisha kuwasiliana na mimi ili kupata punguzo hilo la ada.
NB: unapowasiliana nami tafadhali nukuu jina la chuo kwanza LSC halaf endelea na ujumbe, maswali.. nk.. yako.
TAHADHARI: Sitopokea malipo kutoka kwa mwanafunzi yeyote yule,ada na malipo mengine yanafanyika katika kitengo husika chuoni, ili upate punguzo ni kuwasiliana na mimi nikupe taratibu hisika.
Asanteni
Tanzania National Day Celebrations
9th May 2008..

Nyumba yateketea kwa Moto
Sinza..
Moto mkubwa ambao chanzo chake inadaiwa kuwa shoti ya umeme ukiteketeza nyumba ya Bi Aisha Issa muda mfupi uliyopita maeneo ya Sinza Bamaga, katika tukio hilo Kikosi cha Zimamoto kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kilishindwa kuzima moto huo baada ya gari kugoma kutoa maji na hivyo wananchi kulazimika kujaribu kuuzima kwa kutumia ndoo! Hii ndiyo hali halisi ya 'Faya' zetu za Bongo! Picha na Christopher Lissa/GPL
Mafua ya Kuku Janga
la Taifa..
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akishuhudia wakati Kuku akitolewa damu kwa ajili ya kupimwa kama ana maambukizi ya ugonjwa wa mafua makali ya ndege,katika sherehe ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Tahadhali na Udhibiti wa ugonjwa huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.Kulia ni Dk. Chanasa Mpelumbe-Ngeleja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni,Mfugaji wa Kuku Bi Stella Chambo na katikati ni Waziri wa mifugo na uvuvi Mh John Pombe Magufuli.Picha Ofisi ya Waziri Mkuu
------------
SERIKALI imeutangaza ugonjwa wa mafua ya ndege kuwa ni moja ya majanga ya kitaifa yanayoikabili nchi.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizindua mpango tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa mafua ya ndege nchini, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
"Baada ya kutambua tishio la ugonjwa huu ni kubwa na lina athari kubwa, serikali imeamua kutangaza ugonjwa huu ni moja ya majanga ya kitaifa. Kwa maana hiyo serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ugonjwa huo," alisisitiza Pinda.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini kwa kuwa tayari umeenea Kusini mwa nchi ya Sudan.Habari hii na James Magai
Mzee Mzima Bozi Boziana
Kuwasha Moto
Bongo..
Mratibu wa Tamasha la uzinduzi wa albamu mpya ya Akudo Impact a.k.a wazee wa masauti, Bahati Sigh(katikati)akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa albamu ya Impact yenye jumla ya nyimbo nane itakayo zinduliwa Mei 16 ndani ya ukumbi wa diamond jubilee.katika uzinduzi huo pia kutakuwepo na vikundi vya utangulizi kama Jahazi Modern Taarab pamoja na mwanamuziki aliyewahi kuwika sana miaka ya nyuma kutoka Congo (DRC) Mzee Mzima Bozi Boziana
MSAADA KWENYE TUTA...
*SHERIA BAADA YA UFISADI

JAMANI KUULIZA SIO UJINGA MIMI SI MWANASIASA KWA UNDANI NATEGEMEA KURUDI HOME BONGO ANYTIME THIS MONTH NA NIMEPATA KAZI SERIKALINI NILIKUJA FOR INTERVIEW MIEZI MICHACHE ILIYOPITA SASA ETI MFANO KAMA MIMI NIMEKAMATWA NA KASHFA YA UFISADI SAWA NIKAAMUA KUJIUDHURU INA MAANA BADO NAWEZA KUCHUKULIWA HATUA AU NDIO BASI SO LITAKUWA BWEEEE.JAMANI TUAMBIENI ILI WATU TUWE MAKINI.
MARTHA.
MAISHA BORA KWA KILA
MTANZANIA?
Mamboz Mkuu,
Maisha bora atayapata wapi na lini Huyu mwananchi anayeiishi kwenye hii nyumba na ikiwa baadhi ya viongozi wanaowategemea wamletee hayo maisha bora Mabilioni ya Shilingi wao Wanaita Vijisentiiii!, Tutafika kweliii???
Shukrani
Mdau
xxxxxx
Baraza la China na
Afrika..
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Sshirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini,Oscar Fernandez Taranco, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano kati ya Baraza la China na Afrika mkoani Arusha jana. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango,Mustafa Mkulo na kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania Emmanuel Ole Naiko.
--------------
MAKAMU wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, amewataka wawekezaji zaidi kutoka China, kuwekeza barani Afrika.
Akifungua mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa China na Afrika katika hoteli ya Ngurdoto jana, Dk Shein alisema kuwa, kuna maeneo mengi yanayohitaji uwekezaji mkubwa barani Afrika, ikiwamo sekta ya Kilimo, Madini na Miundombinu.
Dk Shein alifafanua kuwa, katika sekta ya miundo mbinu pekee barani Afrika, kunahitajika uwekezaji wa wastani wa Dola za Marekani 20 bilion.

Vunja Mbavu...

Mazishi Ya Kichaga

----------------

Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yao aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.

Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasi kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza! Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna hii: "Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Machame, katika nyumba ya ukoo.

Samahani sikuweza kuja na mwili kwani nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi huu. Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe. Mgawane hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi. Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili ya mtoto mkubwa wa Mushi.

Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya watoto wa Urassa na Kwayu, natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu. Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya Manka, na zinazobaki ni za watoto wake.

Hizo jeans mpya 2 ambazo mama amezivaa ni za wavulana. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni zawadi ya Koku kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti Rebeka, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.

Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana. Dada yenu mpenzi,

Mama Manka

Jean ping M/kiti Mpya wa
Kamisheni
AU..
Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa afrika (AU) aliyemaliza muda wake profesa alpha oumar konare ambaye leo kakabidhi madaraka hayo kwa Mh. Jean Ping addisababa Ethiopia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia makabidhiano rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa mataifa aliyemaliza muda wake Alpha Oumar Konare(kushoto) kwenda kwa Mwenyekiti Mpya wa kamisheni hiyo Mr.Jean Ping kwenye makao makuu ya Umoja wa Africa,Addis Ababa Ethiopia mchana huu.
Kipanyaa..
Umesikia Hiii ...?
Pichani ni moja kati ya vibao Maalum vilivyopo jijini Dar es salaam vinavyobeba majina ya mitaa husika,Picha juu ni moja kati ya vibao hivyo kilichopo Upanga Street kilichotakiwa kusomeka kama Kisutu Street lakini cha ajabu ni kwamba hivi sasa kimebadilishwa jina na kuitwa 'Pramukh Swami' na watu wasiojulikana kama muonavyo pichani.hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Sebastian Mrindoko ni kwamba Mamlaka husika za jiji la Dar es Salaam wameonyesha kushanganzwa na hatua hiyo ya mtu kujichukulia sheria mkononi na kwa kubadilisha jina la mtaaa.
--------
THE Dar es Salaam City Council has expressed alarm at unsanctioned changes to street names in the central business district being casually done by some residents without the knowledge or approval of relevant authorities.
There is increasing evidence of traditional street name signposts being pulled down and replaced with new sign posts displaying decidedly strange names all over the city and its suburbs. One famous street name in the city was even changed to a new foreign name representing a Hindu religious leader.
Reacting to the situation, DCC Director Bakari Kingobi warned that it was against the city’s by-laws for anybody to change street names without authoritative approval. And according to Kingobi, the Dar es Salaam City Council is the sole authority when it comes to naming streets in the metropolis. ’’It therefore goes without saying that anybody who unilaterally changes street names without our approval, is breaking the law.Habari hii na Sebastian Mrindoko.
Rostam Azizi alishitaki Gazeti la
Mwana Halisi..

MFANYABIASHARA maarufu nchini,Rostam Azizi Pichani,amemshitaki Mhariri wa gazeti la kila wiki la MwanaHalisi na wachapishaji wake akitaka alipwe Sh bilioni tatu kwa kuchapisha habari zinazomkashifu zikimhusisha pamoja na mambo mengine, kashfa ya Kampuni ya Richmond.
Rostam ambaye pia ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wiki iliyopita, akimtumia wakili Kennedy Fungamtama. Licha ya kutaka alipwe kiasi hicho cha fedha, Mbunge huyo pia anaiomba Mahakama kutoa amri ya muda kulizuia gazeti hilo, wakala wake au yeyote kuchapisha habari zinazomkashifu.
Zaidi ya hayo, mfanyabiashara huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Kamati Kuu, anaiomba Mahakama iliamuru gazeti hilo kumwomba radhi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo kwa uzito uleule au zaidi baada ya hukumu yake.
Pia anaomba alipwe gharama za kesi. Rostam anadai kuwa gazeti hilo la MwanaHalisi lilichapisha habari za uongo na za kumkashifu katika toleo lake namba 084 la Februari 13 hadi 19, mwaka huu, chini ya kichwa cha habari, “Richmond ya Rostam Azizi, Ndiye aliyeileta nchini.” Kulingana na mfanyabiashara huyo, kichwa hicho cha habari pamoja na habari yenyewe, zinaonyesha kuwa yeye ni mdanganyifu, asiye mwaminifu, mtoa rushwa na anayetenda matendo maovu na mtu anayeshiriki katika mambo ya udanganyifu.
Rostam anadai kuwa licha ya kuweza kupatikana kwa taarifa sahihi na za wazi kwa urahisi na kwamba kwa njia yoyote ile hajashiriki katika matendo hayo maovu, gazeti hilo liliendelea na kampeni chafu dhidi yake katika toleo lake la 085 la Februari 20 hadi 26, mwaka huu. Anadai kuwa gazeti hilo linadaiwa kuchapisha habari nyingine kwenye ukurasa wa pili chini ya kichwa cha habari, “Kikwete amtosa Lowassa” likimhusisha na biashara zake na kampuni yake, kwamba ni mtu anayefahamika kwamba anaweza kubadilisha ukweli kukidhi matakwa yake.
Mbunge huyo analituhumu gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari kama hizo katika toleo lake la 087 la Machi 5 hadi 11, mwaka huu na toleo la 093 la Aprili 16 hadi 22, mwaka huu likimwonyesha kuwa si mtu muadilifu na anatumia vibaya nafasi yake kwa maslahi yake binafsi. Mfanyabiashara huyo analalamika kuwa maneno hayo yalikuwa na nia ya kumchafua katika biashara na kazi yake kama Mbunge; hivyo kuharibu wasifu, tabia, uadilifu na hadhi yake na kuonyeshwa kwenye jamii kuwa ni mtu wa kashfa, asiye na maana na mdanganyifu.
Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, amejijengea hadhi kama raia mwema, mfanyabiashara, mwanasiasa na mtu wa kuaminika kwa miaka mingi na kutokana na kashfa hiyo, amevunjiwa hadhi mbele ya jamii. Mbunge huyo amedai kuwa anastahili kulipwa kutokana na udhalilishaji huo kwani hadhi yake imeshushwa kiasi cha kuathiri biashara na kazi yake kwa kiwango cha kushindwa kuendesha kazi na biashara yake kwa urahisi.Habari hii na Faustine Kapama.Picha na Salum Mnette
Ridhwan..
Mtoto wa Rais Ridhiwan Kikwete,akivuka viti kutafuta sehemu muafaka ya kukaa ili aweze kushuhudia gwaride maalum la Sherehe za Miaka 44 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
MATOKEO YA KURA ZA
MAONI..
Matokeo ya kura ya maoni kwa wiki lililopita pale FotoBaraza ni haya hapa.
Kama kawaida kuna kura nyingine wiki hii.
Pamoja katika mapambano ya teknolojia.
Bob Sankofa
Muanzilishi wa FotoBaraza.

Sikiliza Clouds FM LIVE

Nifwate Kwenye Twitter

Sheria Ngowi Designs Online Bookings

Google+ Badge

Google+ Followers

Followers

Translate

Blackberry Application


A.V.I.D


Follow by Email

Blog Archive

Mimi na Tanzania

Skylight Band

Grooveback


How to make a Website