Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamiii Mhe.Dkt. Seif Rashid(kushoto)na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge Nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Leo  Aprili 14, 2014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma,Aprili 15, 2014.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na  Waziri wa Nchi Katika Idara  ya Nishati  na Mabadiliko  ya Tabia Nchi wa Uingereza, Mhe.  Gregory Baker (Minister of State at the Department of Energy and Climate Change), Ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 14, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadaye kufanya mazungumzo na Waziri wa  Nishati na Mabadiliko ya tabia Nchi wa Uingereza Mhe Greg Baker Ikulu jijini Dar es salaam leo April 15, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Waziri wa  Nishati na Mabadiliko ya tabia Nchi wa Uingereza Mhe Greg Baker Ikulu jijini Dar es salaam leo April 15, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano linalohusu Mkakati wa Kimataifa wa Kuboresha Miundombinu katika Ukanda wa Kati (Central Transport Corridor) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo April 15, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kongamano linalohusu Mkakati wa Kimataifa wa Kuboresha Miundombinu katika Ukanda wa Kati (Central Transport Corridor) baada ya kulifungua  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo April 15, 2014.Picha na IKULU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, na baadhi ya waombolezaji wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo, Aprili 15,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwanamuziki mkongwe, Kassim Mapili, na baadhi ya waombolezaji wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo, Aprili 15, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo Aprili 15, 2014. Kulia ni Mjane wa marehemu, Pili Binti Saidi Kitwana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanafamilia wa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo Aprili 15, 2014. Kulia ni Mjane wa marehemu, Pili Binti Saidi Kitwana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji katika msiba wa Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam, leo Aprili 15, 2014 kwa ajili ya kuaga kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko
 Baadhi ya wasanii wakijumuika na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Gurumo.
 Sehemu ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehu wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu.
read more
Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja  toka Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Edward Terry Kulia akizungumza na waandishi wa habari  leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo  juu ya mpango wa bohari hiyo kupanua maghala  ya kuhifadhi Dawa na Vifaa  tiba kama moja ya hatua za kuboresha huduma zinazotolewa na Bohari hiyo . Kushoto ni Mkurugenzi  wa Manunuzi wa Bohari hiyo  Bw. Heri Mchunga.
-- 
Na Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yajipanga kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa uhakikika katika hosipitali zote za umma hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja wa Bohari ya dawa (MSD) Bw.Edward Terry  wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza Terry amesema kwa hivi sasa Bohari ya Dawa imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa dawa zinafika kwa wakati katika  maeneo yote zinakohitajika  kwa kuweka mfumo mzuri unahakikisha kuwa  dawa zikifika  zinatumika kwa wananchi waliokusudiwa .
read more
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi Makaazi,Maji na Nishati, katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar  leo asubuhi,.Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar
 Afisa  habari wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bestina Magutu( kulia)akiwa tambulisha  Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa wahariri wa vyombo vya Habari nchini  katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Peacoco jijini Dar es Salaam.ikiwa ni mahususi kwa wahariri vyomba mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi  akisisitiza jambo  kabla ya kuaza mkutano na wahariri wa vyombo vya habari na Mamlaka hiyo , wanaomsikiliza (wapili  kushoto) ni Inspekta Mwanadamizi  Idara ya Udhibiti  wa  Mamlaka ya Anga Tanzania, Mutesigwa Mango ,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti  Masuala ya Anga Julius Kamhabwa  na Afisa  habari wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bestina Magutu( kulia) Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Peacoco jijini Dar es Salaam,ukiwa na lengo la kutoa ufafanuzi  na taratibu za mamlaka hiyo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali nchini.
Inspekta  Mwanadamizi  Idara ya udhibiti Maswala ya Anga,Mutesigwa Mango ,akifafanua jambo  kuhusiana na ajira za Maarubani  na wahudumu wa ndege  hapa nchini  wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliohusu  kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo,Mkuatano huo ulifanyika katika hoteli ya Peacoco  jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi .Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti  Masuala ya Anga Julius Kamhabwa.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Masuala ya Anga, Julius Kamhabwe akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa  katikaMkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,ambao ulilenga kufafanunua kuhusu kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi  na  Inspekta  Mwanadamizi  Idara ya udhibiti Maswala ya Anga,Mutesigwa Mango.
read more
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wacheza ngoma na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi tarehe 14.4.2014
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo tarehe 14.4.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bahi.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi tarehe 14.4.2014.
read more
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Philemon Ndessamburo (kushoto) na James Mbatia (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
]Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sophia Simba (kushoto) na James Lembeli (katikati) na Job Ndugai (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi (Wapili kushoto) wakifurahia jambo katika mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Kificho (wapili kulia) na Haidar Madeweyya .
read more
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akifungua mafunzo ya Ukimwi mahali pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwishoni mwa juma, Semina hiyo iliyoandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii na mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa kwa watumishi hao ilikua na lengo la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu janga la Ukimwi na umuhimu wa Tohara kwa wanaume katika kujikinga na janga hilo. Katika hotuba yake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa hakusita kuonyesha hisia zake kali kwa watumishi watakaohusika katika rushwa za ngono na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali bila ya utetezi wowote kutoka kwake.
Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa Ndugu Daniel Mwaiteleke akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu gonjwa la UKIMWI kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga.
Muwezeshaji wa mada ya magonjwa ya zinaa STD na STI Dkt. Lunyelele akiwasilisha mada yake kwa umahiri mkubwa bila ya kutafunatafuna maneno
read more
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu.

Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union).

Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.

Mambo yote mawili yametusononesha sana sisi Serikalini, na bila shaka yamewasononesha wananchi wanaoipenda nchi yao, wanaowapenda Waasisi wa Taifa letu na kuuenzi Muungano wao.

Madai ya kuonyeshwa Hati ya Muungano yalianza siku nyingi lakini hatukuweza kuamini hali itafikiwa ilipofikia, ambapo wapo watu wanathubutu kudai na kuapa kuwa Hati hiyo haipo.

Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo, ilikuwepo siku zote. Hata hivyo, lazima tukubaliane kuwa zipo Hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama Taifa huru, Jamhuri huru na Muungano huru, ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho. Hati hizo ni pamoja na Hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961, Hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962, na Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. Hati za aina hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika. Kwa kawaida hatuzitoi, tunazifungua ili kuzihifadhi kwa namna yoyote ile.

Lakini sasa maneno yanakua mengi, tuhuma zimekuwa nyingi, dhihaka zimekuwa nyingi, kiasi cha wananchi kuanza kutiwa mashaka iwapo kweli Hati ya Muungano ipo au la.

Hivyo, kwa maagizo na ridhaa ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaleta mbele yenu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyotiwa saini Zanzibar na waasisi wetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume, ili muione na kuwahakikishia Watanzania kuwa yanayosemwa kuwa hakuna Hati hiyo si kweli. Hati hiyo ipo tangu wakati huo, imetunzwa vizuri na waliotutangulia, tumeirithi, na tutaendelea kuihifadhi.

Na, tukiombwa kufanya hivyo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum nina uhakika Rais ataridhia ipelekwe huko ili kuondoa mjadala wa kama Hati ipo au la.

Isitoshe, tufanye utaratibu wa kuweka nakala kwenye Makumbusho ya Taifa ili kila atakayetaka kuiona katika miaka mingine 50 ijayo na kuzidi aione.

Mwisho, narejea kusema kuwa kwa upande wa Serikali tunasikitishwa na kufadhaishwa sana na tuhuma nzito kwamba labda waasisi wetu hawakuwa makini au walitufanyia kiini macho. Hatukutarajia wawepo Watanzania wenzetu, wafikie hapo.

Ni jambo zito. Vile vile hatukutarajia kuwa Serikali itatuhumiwa kuwa haikuwa makini kuhifadhi waliosaini waasisi wetu.

Matumaini yetu ni kuwa baada ya leo tutaendelea na mambo ya msingi kwa mustakabali, umoja na uimara wa Taifa letu badala ya kuchochea hisia kuwa Muungano wetu hauna msingi imara wa kisheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Aprili, 2014
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.Picha na Freddy Maro-IKULU


  
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.
read more

 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma ujumbe ulioandikwa na wanakijiji cha Mnyagala ambao waliusimamisha msafara wake na kumpa ujumbe wa kero yao ya kutokuwa na barabara na zahanati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mnyagala wilayani Mpanda na kuwapa majibu namna ambavyo kero zao zitaisha kwa utaratibu ambao Serikali,Mbunge na wananchi hao watashirikiana kumaliza hizo kero kwa makubaliano na uataratibu uliowekwa baina ya Vijiji na serikali mkoani Katavi.
read more

Marehemu  Muhidin Maalim Gurumo Enzi za Uhai Wake
--

 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini Maalimu Ngurumo. 

“Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.”


Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.


Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


Imetolewa na
Godfrey Mngereza
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionyesha kwa Waandishi wa Habari Hati ya Muungano Kwenye Mkutano Wake na Waandishi wa Habari LEO
--
Ikulu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue  imeionesha Hati ya Muungano Mbele ya Waandishi wa habari Jijini Dar es Salam Leo, Pamoja na Mambo mengine Balozi Ombeni Sefue Amesema Hati hiyo na ipo imehifadhiwa mahali ambapo wananchi hawapaswi kufahamu kwa sababu za kiusalama.

*Habari zaidi Baadae

Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.
Msanii wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa washiriki 15 bora hapo kesho.
read more

Nifwate Kwenye Twitter

Blackberry Application


A.V.I.D


Follow by Email

Blog Archive

Sheria Ngowi Designs

Mimi na Tanzania

Hakielimu

Zane Microfinance

Zane Microfinance

Skylight Band

Flavanite

Flavanite

Grooveback


Followers

How to make a Website